Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa kuingilia mawasiliano ya watu na kuyarusha mitandaoni ni jambo gumu sana ukilitafakari.
Hatua hiyo inakuja baada ya kuzuka tabia ya kuzuka kuenea sauti mitandaoni zinazodaiwa kuwa ni za wanasiasa jambo ambalo mpaka sasa hakuna anaejua kuwa ni kweli au lah.
"Kuingilia mawasiliano ya watu na kuyarusha mitandaoni ni jambo gumu sana ukilitafakari,lina ondoa heshima na utu,kwani ktk maongezi ya simu kuna zaidi ya siasa,kuna mapenzi,biashara na mambo ya familia,kushangiliia jambo hili ni kukosa utu na adabu kwa kiwango cha hali ya juu." ameandika Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Lema ni Mbunge ambaye amesimamishwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge mpaka ambapo ataanza kuhudhuria mwakani.
No comments:
Post a Comment