Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amelishangaa Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kwa kuwa 'vigeugeu' baada ya kubadili uamuzi wa kuzipeleka moja kwa moja raundi ya kwanza timu zilizotinga hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita
Awali CAFwalitoa taarifa kuwa timu nane ikiwemo Simba hazitacheza hatua ya awali ya michuano hiyo inayoanza mapema sana mwaka huu mwezi wa nane
Hata hivyo ni timu tatu tu ambazo zitaanzia raundi ya kwanza ambazo ni timu mbili zilizotinga fainali, Esperance na Wydad Athletic pamoja na TP Mazembe
Uamuzi huo umevuruga ratiba ya mabingwa hao wa Tanzania Bara ambao ndio kwanza wako Afrika Kusini wakikiandaa kikosi chao
Aussems amesema atalazimika kufanya mabadiliko ya program za mazoezi ili kikosi chake kiwe tayari kwa mchezo wa August 09 dhidi ya UD do Songo nchini Msumbiji
cut
"Hatukuwa tumejiandaa na ratiba hii kwa sababu tulifahamu tungeanzia raundi ya kwanza, lakini inashangaza ni timu tatu tu ambazo zimepewa nafasi hiyo," amesema Aussems
"Tutalazimika kubadili program za mazoezi ili tuweze kuwa tayari kwa mchezo huo"
"Tunaweza tusiwe tayari kwa asilimia 100 kwenye mchezo wa kwanza, lakini nina uhakika kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Tanzania tutakuwa tumeiva"
No comments:
Post a Comment