Mchezo huo maalumu kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wao unatarajiwa kuchezwa saa kumi jioni ambapo utatanguliwa na mechi kati ya Bongo Fleva na Bongo Movi na mavetenali wa Yanga na Pamba.
Akizungumza Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Hamasa wa klabu hiyo, Deo Muta alisema mchezo huo utakuwa katika viingilio vitatu ambapo kiingilio cha chini ni Sh 5,000 kwa mzunguko wa orange.
Muta alisema kwa upande wa VIP B kiingilio kitakuwa Sh 30000 wakati VIP A itakuwa ni Sh 100,000.
"Tunawaomba mashabiki wetu na wadau wa soka kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia usajili bora uliofanywa na klabu yetu ikiwa ni sambamba na burudani kutoka kwa wasanii na wakongwe wa ligi."
"Kutakuwa na wakongwe waliofanya kazi kubwa kipindi hicho Yanga ambao naamini kuwa watu hawawafahamu tutaweka majina kwenye jezi zao watakazovaa wakati wa kucheza ili kuondoa tabu kwa mashabiki kushindwa kutambua nani anamiliki mpira," alisema Muta.

No comments:
Post a Comment