Beki mahiri wa Simba Shomari Kapombe amemaliza program binafsi ya mazoezi aliyopewa mwezi uliopita ili kumuweka sawa kabla ya kurejea dimbani
Kapombe sasa yuko tayari kurejea uwanjani na ataungana na kikosi cha Simba ambacho kinatarajiwa kutimkia Afrika Kusini kuweka kambi
Kapombe amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi saba akiuguza majeraha ya kuvunjika mguu aliyopata akiwa na timu ya taifa mwezi Novemba mwaka jana
Alikuwa miongoni mwa wachezaji walioitwa kikosi cha Stars kwa ajili ya Afcon kabla ya jina lake kuondolewa kutokana na sintofahamu iliyojitokeza baina yake na benchi la ufundi kuhusu aina ya mazoezi ambayo alipaswa kupewa
Msimu ujao anatarajiwa kuongoza nafasi ya beki wa kulia hasa baada ya Simba kumtosa aliyekuwa mbadala wake Zana Coulibaly

No comments:
Post a Comment