Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki kuelekea Afrika Kusini kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara pamoja na michuano ya Kimataifa
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Patrick Aussems anatarajiwa kurejea nchini leo kuungana na nyota wa Simba ambao tayari wameanza kuwasili kutoka mapumziko
Simba inatarajiwa kujifua huko Afrika Kusini kwa takribani wiki tatu kabla ya kurejea nchini tayari kwa tukio la SIMBA DAY linalofanyika AUgust 08 ambalo hutumika kutambulisha kikosi
Awali Simba ilikuwa ikaweke kambi Ulaya, hata hivyo muda uliobaki kabla ya kuanza kwa msimu mpya ni chini ya wiki tano hivyo mabosi wa Simba kuamua kubadili kambi hiyo

No comments:
Post a Comment