Mlinda lango Ramadhani Kabwili ametua mkoani Morogoro kujiunga na kikosi cha Yanga kinachojifua na maandalizi ya msimu mpya
Kurejeshwa kwa Kabwili kikosini kunamuweka kwenye hatihati mlinda lango Klaus Kindoki kwani Yanga itakuwa na walinda lango wanne
Awali Kabwili hakuwemo kwenye kikosi cha Yanga cha msimu ujao lakini kuibuka mazoezi kwa mlinda lango huyo kinda, kunamaanisha amerejeshwa
Yanga ina makipa wanne ambao ni Farouq Shikalo, Metacha Mnata, Klaus Kindoki na Ramadhani Kabwili

No comments:
Post a Comment