Miamba ya soka kutoka ligi ya Serie A, klabu ya Juventus imeripotiwa kuwa ipo tayari kumtoa mshambuliaji wao, Paulo Dybala kwa Mashetani Wekundu Manchester United ili kuweza kupata saini ya Romelu Lukaku ambaye pia anawindwa na timu ya Inter Milan.

Wakati dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa Agosti 8, United inahaha kuhakikisha inapata mbadala wa Lukaku endapo ataondoka ndani ya timu hiyo.
Kwa mujibu wa Tuttosport, United inakaribia kufikia makubaliano na Juventus kwa kushuhudia Mbelgiji huyo akitimkia kwa vibibi vizee vya Turin huku Dybala akitua Old Trafford.

Katika ukurasa wa mbele wa Tuttosport siku ya Jumatatu umegubikwa na picha ya Romelu Lukaku inayohusu stori ya kujiunga na Juventus.

Juventus imeripotiwa kutaka kuipiku Inter kwa kumsajili nyota wa United raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku

Ingawaje Inter Milan imekuwa kivutiwa na usajili wa Lukaku katika kipindi chote wameshindwa kutoa pauni milioni 80 kwa United na badala yake wakatoa milioni 54 na kukataliwa.

Lukaku akizungumza na kocha wa Inter Milan, Antonio Conte katika mechi za wiki kadhaa zilizopita jijini Singapore

Dybala akishangilia baada ya kuipatia Juventus bao kwenye mechi dhidi ya Manchester United mchezo wa Champions League msimu uliyopita.
Nyota huyo wa Argentine mwenye umri wa miaka 25, Dybala amefunga jumla ya mabao 78 katika michezo 182 aliyocheza akiwa na Juventus
No comments:
Post a Comment