Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, amewataka askari kuhakikisha wanaongeza mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo ujambazi, vinavyojitokeza hususan katika mkoa wa Geita.
IGP Sirro ameyasema hayo akiwa anazungumza na askari wa kikosi maalum cha kupambana na uhalifu katika mkoa huo.
Wakati huo huo akiwa mkoani Shinyanga, IGP Sirro amewaonya madereva wa pikipiki maarufu bodaboda kuhakikisha wanavaa kofia ngumu (Helmet) wakati wote wanapotumia chombo cha moto, kuwa na leseni sambamba na kuheshimu sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza
kuepukika.
Akiwa mkoani Shinyanga, pia IGP Sirro amekutana na kuzungumza na baadhi ya wananchi wa Shinyanga mjini na kuwataka kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na hasa kwa kutoa taarifa sahihi za uhalifu na wahalifu.

No comments:
Post a Comment