We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, July 5, 2019

Gadiel, Luhende wapishana Jangwani


HUKO Jangwani mambo ni moto, kwani baada ya beki wao wa kushoto, Gadiel Michael kuamua kuwatingisha na kuchomolea Msimbazi, mabosi hao wa Jangwani fasta wakafanya jambo moja kwa kumsajili David Luhende kuziba nafasi yake.
Awali Mwanaspoti la juzi Jumanne lilidokeza kuwepo kwa mipango ya Yanga kumrejesha Luhende Jangwani, ila sasa unaambiwa mpango huo umekamilika kwa Gadiel kupishana na beki huyo mwenye mashuti makali ambaye amesajiliwa rasmi kutoka Kagera Sugar.
Mipango ya Yanga kuzungumza na Gadiel aliyekuwa timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa ikishiriki Fainali za Afcon 2019 ilishindikana baada ya beki huyo kugoma kusaini mkataba aliopewa kabla hata hajatimkia Misri, huku Simba ikitajwa kutibua mambo.
Gadiel alitaka kusaini mkataba mpya kwa Sh 50 milioni na Yanga ikawa tayari kumpa kwanza Sh 30 milioni kisha kummalizi Sh 20 milioni baadaye, lakini kuumwa kwake sikio na Simba kulimfanya awachenge hasa baada ya Mwenyekiti wa Simba, Swedy Mkwabi kutua Misri kuweka mambo sawa na mabosi wa Yanga wakajiongeza fasta kwa Luhende.
Awali Yanga walitamani kumrejesha beki wa kushoto wa zamani wa Tusker Kenya na Singida United anayekipiga Gor Mahia, Shafiq Batambuze, lakini kukamilika kwa idadi ya nyota wa kigeni Jangwani kuliwafanya warejee kwa wazawa na jina la Luhende likapita.

Jina hilo lilitua kwa Zahera akiwa na timu ya taifa ya DR Congo na kutoa baraka zote asainishwe fasta, kwani Haji Mwinyi Mngwali waliyetaka kumbakisha naye aliwadengulia.
Inaelezwa kitendo cha Gadiel kutajwa kuwepo kwenye kikosi cha msimu ujao cha Simba ndiko kulikowapa hasira mabosi wa Yanga kupambana kumrejesha Luhende anayekumbukwa kwa shuti kali alililomtungua kipa Aishi Manula wakati akiwa Mwadui.“Tumewasiliana na Luhende, aliye huru na jana Alhamisi asubuhi tulikutana nae na kwa sasa bado kusaini tu, kwani hatuna namna kwani Gadiel na Mwinyi wote wamezingua,” kilisema chanzo makini kutoka Yanga.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alipoulizwa suala hilo la Gadiel kupishana na Luhende, alisema;
“Kauli yetu tutaitoa baada ya Gadiel kutua nchini kesho (leo) akitokea Misri ili kujua kama atasaini kubaki nasi ama ataondoka Jangwani, kwani tulimpa mkataba kabla hajaenda Afcon, lakini amekuwa akituzungusha.”

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list