We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, July 9, 2019

Dkt. Mpango akabidhiwa gawio la Benki ya Posta


Benki ya Posta Nchini TPB leo imekabidhi gawio la Shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali pamoja na wanahisa wengine kama faida ambayo wameipata kutokana na shughuli zake ikiwa ni mara ya pili mfululizo.

Gawio hilo limekabidhiwa kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango leo katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kupokea gawio hilo, Waziri Mpango ameipongeza Benki ya TPB kwa kuendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki takribani 50 yaliyopo nchini.

"Kwa kweli ni jambo kubwa na la kipekee sana ambalo Benki ya Posta imelifanya, nitoe shukrani za dhati kwa Uongozi wa Benki hii kwa gawio hili la Bilioni moja ambalo mmelitoa kwa Serikali, hii ni mara ya pili mfululizo mmetoa gawio hili na hakika mnastahili pongezi.

"Kutoa kwenu gawio hili kunaashiria kwamba Benki ya TPB imeendelea kufanya vizuri kiutendaji, na hii inatia moyo na kutoa hamasa kwa wanahisa tunaomiliki hisa kwenye Benki yenu," Amesema Dk Mpango.

Dk. Mpango pia ametoa wito kwa Taasisi zingine za umma zinazotaka huduma za kibenki kote nchini na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma za Benki ya TPB.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Dk. Edmund Mndolwa amesema Benki ya TPB imefanya vizuri kwa mwaka jana kwa kupata faida ya Shilingi Bilioni 17 na hivyo kuweza kutoa gawio la Shilingi Bilioni Moja kwa wanahisa zake na Serikali.

"Najisikia daraja kusimamia Benki inayoendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki yaliyopo sokoni, ni matumaini yetu kwamba tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Rais wetu Dk Magufuli katika kuifanya Tanzania inafikia uchumi wa kati," Amesema Dk Mndolwa.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list