We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, July 9, 2019

Dk Kigwangalla asema wanaopinga Stigler’s Gorge watafanyiwa fujo, kubanwa mbavu


Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzamia, Dk Hamis Kigwangalla amesema wanaharakati wanaopinga mradi wa kufua umeme wa Stigler’s Gorge watafanyiwa fujo zisizoumiza kabla hawajafika kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli lakini ikibidi watabanwa mbavu.

Dk Kigwangalla  ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 9, 2019 wakati wa uzinduzi wa Hifadhi Taifa ya Burigi- Chato mkoani Geita ambayo imetokana na kuunganishwa kwa mapori ya akiba ya Kimisi, Burigi na Biharamulo.
Amesema Rais Magufuli ndiye mhifadhi namba moja anayetekeleza kwa vitendo na hahitaji mtu yeyote kutoka ndani na nje ya nchi kuja kutufundisha namna ya uhifadhi.
“Ulipotia nia ya kuwekeza katika mradi wa kufua umeme katika mbuga ya Selous kuna wanaharakati walianza kupiga kelele wa ndani na wa nje kana kwamba hifadhi ni ya kwao au wanajua kuhifadhi kuliko wewe,” amesema
Amesema mradi ule ni wa siku nyingi hata wakati mbuga hiyo inaomba kuidhinishwa kuwa miongoni mwa urithi wa dunia UNESCO walielezwa kuna mpango wa mradi huo na waliridhia hivyo hata baada ya mradi hadhi itaendelea kuwa ile ile.


“Wanaharakati ambao wanapenda kujionyesha...wakiendelea kuleta chokochoko kupitia mawakala wao mbalimbali wa kisiasa na harakati tutaanza nao sisi kabla ya kukufika kwako, tutawafanyia fujo zisizoumiza ikibidi kuwabana mbavu tutafanya hivyo,” amesema Dk Kigwangalla.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list