Hatma ya beki Andrew Vicent 'Dante' kuendelea kubaki Yanga iko mashakani kutokana na uamuzi wake wa kugoma kuingia kambini mkoani Morogoro
Inaelezwa uongozi wa Yanga uko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa beki wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha wa timu hiyo
Chikupe na Abdul waligoma kuingia kambini na kikosi cha Yanga ikielezwa wana madai ya fedha za usajili
Aidha taarifa zilizopatikana jana zimebainisha kuwa suala la Abdul limepatiwa ufumbuzi na wakati wowote atajiunga na wenzake mkoani Morogoro
Kumekuwa na taarifa kuwa Dante huenda akaibukia klabu ya Lipuli Fc ambayo imeonyesha nia ya kutaka kumsajili
Dirisha la usajili litafungwa Julai 31, siku tano zikiwa zimesalia
Uongozi wa Yanga umeweka msisitizo kwa wachezaji wake kuwa na nidhamu na kutimiza wajibu wao wakati changamoto zao zinashughulikiwa
Msimu uliomalizika Yanga ilimsimamisha na baadae kumuondoa kikosini mlinda lango Beno Kakolanya baada ya kugoma
Beki Gadiel Michael aliyekuwa anasuasua kusaini mkataba mpya nae alikumbana na msimamo mkali wa Yanga baada ya kuachwa na nafasi yake kuchukuliwa na Mwarami Issa 'Marcelo'
Gadiel na Beno wote wamesajiliwa na Simba

No comments:
Post a Comment