Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amewatolea uvivu waamuzi pamoja na wasimamizi wa mchezo wa leo usiku dhidi ya Brazil, Kwa kuwambia kuwa walishindwa kuchezesha mchezo huo na kuwapendelea zaidi brazil.

Messi amesema kuwa timu yake ilikuwa bora uwanjani kwa muda wote lakini waamuzi walifanya maamuzi ya ajabu yaliyopelekea Argentina kufungwa.
“Tuliwazidi kila kitu uwanjani, Ila ni upumbavu tu wa waamuzi wetu wa mchezo,“amesema Messi mapema baada ya mchezo huo kumalizika na kuongeza.
“Walipata goli la kwanza mapema kipindi cha kwanza, Na sisi tulitakiwa tupate goli kupitia kwa faulo aliyochezewa Aguero ile ilikuwa ni penati, Lakini kwa upumbavu wa waamuzi na ni jambo la kushangaza hawajaenda hata kuangalia VAR,“ameeleza Messi kwa uchungu.
“Upambavu huo uliendelea karibia kwenye mchezo wote, Kila wao (Brazil) wakicheza rafu filimbi haipigwi tukiwagusa wao kidogo refa anapuliza filimbi. Hii ilitutoa kwenye mchezo,“amemaliza Messi kwa kuisifia timu yake.
“Hatuna sababu ya kujitetea, Timu yetu imecheza vizuri zaidi yao ila tuna sababu ya kuongea ukweli waamuzi wameibeba saba Brazil tunajua wana sababu zao na tunaamini shirikisho la soka America Kusini (CONMEBOL) watafanyafanyia kazi haya ninayoongea,”amesema Messi.
Alfajiri ya kuamkia leo Jumatano Julai 3, 2019, timu ya taifa ya Argentina imekubali kichapo cha goli 2-0 dhidi ya Brazil kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Copa America.
No comments:
Post a Comment