We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, June 8, 2019

Zahera kumaliza usajili Misri

Yanga imeanza usajili wake mapema tu kuhakikisha inakuwa na kikosi imara kitakacholeta ushindani kwenye michuano ambayo timu hiyo itashiriki msimu ujao
Wakati inaanza usajili, taarifa ya kushiriki michuano ya CAF haikuwepo lakini mambo huenda yakabadilika baada ya mabingwa hao wa kihistoria kuhakikishiwa nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao baada ya CAF kuongeza idadi ya timu kwa Tanzania kutoka mbili na kuwa nne
Inaelezwa kocha Mwinyi Zahera ataitumia michuano ya AFCON 2019 inayoanza Juni 21 nchini Misri kupata wachezaji wa kujaza nafasi zitakazokuwa zimebaki
Mpaka sasa wachezaji wa kigeni ambao wanatajwa kusajiliwa na Yanga ni Lamine Moro, Patrick Sibomana, Issa Birigimana, Sadney Urikhob, Mustapha Suleyman, Maybin Kalengo, Farouq Shikalo na Papi Tshishimbi
Zahera amesema baada ya kupata nafasi hiyo ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao, wanahitaji kuwa na kikosi imara kitakachokuwa na ushindani
Amewataka wadau wa klabu hiyo waendelee kuisapoti timu kwa kushiriki kikamilifu Harambee ya Kubwa Kuliko itakayofanyika Jumamosi ijayo ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
"Bado tunaendelea kuangalia wachezaji wa kiwango cha juu, tutaangalia Afcon na hata CHAN, tuna uwezo wa kusajili mchezaji yeyote yule, tunawaomba mashabiki na wanachama wa Yanga waendelee kuisapoti klabu yao, wajitokeze kwenye Harambee ya kuichangia timu ili tupate fedha zaidi za kusajili" amesema

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list