Real Madrid itafikiria kuwasaini kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, badala ya kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba. (Independent)
Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri atatia saini kandarasi ya miaka mitatu ili kuchukua wadhfa wa kuifunza Juventus wiki ijayo (Guardian)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Eric Dier, 25, anafikiriwa na Manchester United kukaza safu ya kati Katina kikosi cha kwanza cha wachezaji 11. (Times - subscription required)
Barcelona imekataa ripoti kwamba itamnunua kipa Gianluigi Buffon baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41- kutangaza kwamba ataondoka Paris Saint Germain mwisho wa msimu huu (Mundo Deportivo - in Spanish)
Buffon anataka kustaafu katika soka baada ya kushinda dhahabu katika michezo ya Olimpiki akiichezea Itali katika mashindano hayo yatakayofanyika nchini Japan(Gazzetta dello Sport, via Mail)Barcelona itamwania mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 21, iwapo itashindwa kumsajili Antoine Griezmann au Neymar. (Mail)Atletico Madrid inataka kumsajili beki wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 28, ili kumrudisha nyumbani (Goal)
Mchezaji wa Fulham na Uingereza Ryan Sessegnon, 19, ameambia klabu hiyo hatosaini kandarasi mpya na kwamba anaelekea Tottenham (Guardian)
Liverpool itashindana na Tottenham na Manchester United katika kumsaini kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 24 na raia wa Ureno Bruno Fernandes kutoka Sporting Lisbon. (Record, via Mirror)
Winga wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe atakataa ombi la kucheza katika ligi ya Uingereza na badala yake kuelekea Bayern Munich. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ananyatiwa na Liverpool na Manchester United. (Sun)
Arsenal wameambiwa watalazimika kuilipa Sampdoria £44m ili kumnunua mchezaji mwenye umri wa miaka 22-beki wa Itali Joachim Andersen na winga wa Ubelgiji Dennis Praet, 25. (Star)West Ham na Arsenal note wanamtaka king wa kati wa Eibar na Uhispania Joan Jordan, 24. (Marca - in Spanish)
West Ham wanamnyatia mchezaji wa Newcastle na nyota wa Uingereza 21 Isaac Hayden, 24. (Star)
Everton imejiunga na Arsenal Katia harakati za kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 27 beki wa Togo defender Djene Dakonam kutoka Getafe. (Marca - in Spanish)
No comments:
Post a Comment