Na Clavery Christian, Biharamulo
Ardhi haiongezeki ila sisi binadamu tunaongezeka, DC Biharamulo amewataka wanachi wa kijiji cha nyantakara kata ya nyantakara wilayani biharamulo kuacha tabia ya kuvamia maeneo kwa kisingizio cha kwamba watu wamekuwa wengi maeneo waliyom hayawatoshi.
Mkuu wa wilaya Biharamulo, Bi, Sada Malunde alisema hayo katika mkutano wake na wanakijiji cha Nyantakara wa kuwasilisha mpango wa matumizi bora ya aridhi utakao saidia kupunguza uharibifu wa mazingira na miundo mbinu huku wanakijiji wakijifunza kutumia eneo dogo kupata mazao mengi.
Bi, Sada alisema kuwa serikali haitaweza kuongeza ardhi kwa sababu kila siku binadamu tunazidi kuongezeka hivyo inachofanya saizi nikuleta mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Baadhi ya wanakijiji walisema kuwa mpango huo utaweza kusaidia kuondoa kero na migogoro ya ardhi nakuiomba serikali kuhakikisha inapeleka mpango huu katika vijiji vingine.
Kwa upande wake Meneja wa wakala wa misitu wilaya Biharamulo amesema kuwa mpango huu utasaidia hasa vijiji vinavyozunguka hifadhi za misitu kuacha migogoro ya mipaka ya vijiji na hifadhi ambapo wanakijiji wataweza kujua wapi wanaishia na wapi hawaruhusiwi kulima au kulisha mifugo yao.
No comments:
Post a Comment