Mchezaji ghali zaidi duniani, Neymar hatimaye ameamua kuonyesha majeraha yake ambayo ameyapata mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mchezo wa kirafiki kati ya timu yake ya taifa ya Brazili dhidi ya Qatar.
Nyota huyo wa klabu ya Paris Saint-Germain ameonyesha jeraha hilo kupitia akaunti yake ya kijamii ya Instagram kupitia Insta Story, ambapo mguu wake wa kulia ukionyesha namna alivyopata majeruhi “ankle.”
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 27, alipata ankle hiyo dakika za mapema tu wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 0 dhidi ya Qatar siku ya Jumatano, ambapo alisaidiwa kutoka nje ya uwanja kupitia madaktari wa wachezaji wa timu huku akonekana akitokwa na machozi.
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Tite alinukuliwa akisema majeraha ya nyota huyo sio makubwa ingawa Neymar ameonekana akitolewa nje ya uwanja kwa msaada wa madaktari huku akiwa amevalia piopio.
Kutokana na uzito wa jeraha “ankle” alilopata Neymar hatukuwa kwenye hali nzuri na huwenda kuchelewa kuwa sawa kimwili kwaajili ya michuano ya Copa America mwaka 2019. Kwa upande wa timu ya taifa tayari umethibitisha kukosekana huduma yake kwenye mechi dhidi Bolivia Juni 14.
No comments:
Post a Comment