Uongozi wa Yanga umepanga kuwafanyia sherehe ya kuwaaga nyota wake ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao
Kutokana na changamoto zilizoikumba timu hiyo msimu uliomalizika, wachezaji wengi walijitoa kwa moyo licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi
Uongozi wa timu hiyo umeona halitakuwa jambo jema kuwaacha hivi hivi bila ya kutambua mchango wao
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebelea amesema wachezaji hao wataondoka kwa kupewa heshima wanayostahili baada ya utumishi wao
"Timu yetu imecheza kwa kuungaunga msimu huu ni vyema kuwapongeza nyota wetu waliotufikisha hapa tulipo"
"Tarehe ya kuwaaga nyota hao itatangazwa mara baada ya uongozi kukabidhiwa ripoti ya mwalimu ili kufahamu ni nyota gani hatutakuwa nao," Mwakalebela amenukuliwa na Mwanaspoti
cut
Wachezaji wanaotajwa kutokuwa kwenye mipango ya kocha Mwinyi Zahera kwa ajili ya msimu ujao ni pamoja na Pius Buswita, Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko, Beno Kakolanya, Said Makapu, Said Mussa, Matheo Anthony, Juma Mahadhi na Burhan Akilimali
Aidha baadhi ya wachezaji huenda wakatolewa kwa mkopo kujiunga na timu nyingine
Wanaotajwa kuwa katika mpango huo ni pamoja na Deus Kaseke, Jaffar Mohammed, Mrisho Ngasa, Abdallah Shaibu, Mohammed Issa 'Banka' na Yusufu Mhilu ambaye msimu uliomalizika aliitumikia Ndanda Fc kwa mkopo
Hivi karibuni Zahera alisema kuwa kikosini kwake kuna wachezaji 19 ambao wamemaliza mikataba na atafikiria, anaweza akawaacha wote na kusajili wengine
No comments:
Post a Comment