Bashungwa ametoa maagizo hayo leo Jumamosi Juni 28, 2019 wakati wa ziara ya kikazi mkoani humo ya kutembelea viwanda vya 21th Century (Polyester), Mazava na Tumbaku Cha TTPL.
Amesema Serikali mara baada ya kubinafsisha viwanda vyake mwaka 2005, adhima yake ilikuwa ni kuhakikisha viwanda vinafanya kazi kwa kuzingatia mikataba iliyopo.
Waziri Bashungwa amesema ni ya kusisitiza hilo suala la ajira ili iweze kuchangia kwenye pato la nchi lakini kubwa zaidi ni wakulima kunufaika.
Pia, waziri huyo amepongeza kiwanda viwanda vya 21th Century (Polyester) kwa namna inavyotumia maganda ya korosho katika kuendesha mitambo yao ambapo akielekeza uongozi wa Shirika la Viwanda vidogo Tanzania (SIDO) kufika katika kiwanda hicho kwa nia ya kuhakikisha unaifanya ushirikishwaji na viwanda vinavyobangua Korosho.
"Tukiweza kulima pamba na korosho naimani kutakuwa na matokeo makubwa kwani njia mnayotumia wakati mnatengeneza nguo kwa kutumia nguvu ya maganda ya Korosho kuendesha mitambo itasaidi," amesema.
Kwa upande wake, ofisa utumishi katika kiwanda hicho, Doris Kiwango amesema kama kampuni iliamua kutumia maboila yanayotumia makaa ya mawe na mabaki ya mazao ya mashambani ikiwemo maganda ya Korosho.
Kiwango amesema kutumika kwa maganda hayo imesaidia na kupunguza gharama za kupata mvuke unaotumika kwa wingi sehemu mbalimbali za uzalishaji ikilinganisha na gharama za kupata mvuke.
No comments:
Post a Comment