We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, June 29, 2019

Watanzania tisa wameuawa, IGP “wanauliza wewe Mtanzania ukijibu ndio wanakuua”

Raia tisa wa Tanzania pamoja na raia wawili wa Msumbiji wameuawa na watu wasiojulikana huku Watanzania wengine sita wakijeruhiwa katika kijiji cha Mtole kilichopo upande wa Msumbiji mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchni, IGP Sirroamefika mkoani Mtwara kufuatilia tukio hilo lililotokea June 26, 2019.
“Nasikitika kwa vifo vya Watanzania, hatutokuwa na muhali na Muuaji akipatikana hata akitangulia mbele za haki kwangu ni sawa, nitajibu mbele za haki, uwezo tunao tutatumia Interpol na sheria zilizopo kuhakikisha waliofanya mauaji wanapatikana wakiwa salama au wamefariki”-IGP Sirro
“Na bahati mbaya taarifa tulizopata wanaofanya haya mauaji wanazungumza Kiswahili kizuri sana, wengi ni wale waliokimbia huku kwetu baada ya kupata moto mkali, hawa watu wa hovyohovyo wanauliza wewe Mtanzania ukijibu ndio wanawapiga risasi” – IGP Sirro
“Timu zetu za oparesheni zinapita maeneo mbalimbali kuhakikisha maeneo yetu, Mtwara yetu inakuwa shwari, Kijiji ambacho wameletwa kule ambako wamezikwa nimetoa maelekezo tutakuwa na doria ya kutosha maeneo yale mpaka hali itakapokuwa shwari”– IGP Sirro

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list