Wananchi wa kijiji cha Itunduma wilayani Njombe wameazimia kumfukuza kijijini hapo Ang'emelye Wikechi, kwa kile kinachoelezwa kuwa amekuwa ni chanzo cha uvunjifu wa amani kijijini hapo.

Hatua hiyo inakuja kufuatia wananchi hao Kugoma kufanya shughuli za maendeleo wakimshinikiza mkuu wa wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri, kufika kijijini hapo ili kutoa tamko la mwisho juu ya raia huyo.
Moja ya tuhuma kubwa zilizoelekezwa kwa Wikechi na wanakijiji wenzake, anadaiwa kunyang'anya na kujimilikisha ardhi ya kijiji na maeneo mengine ambayo ni mali ya taasisi.
Pamoja na hayo Ang'emelye anadaiwa kutishia maisha ya wananchi wenzake ambao wamekuwa wakihoji juu ya maovu anayofanya kijijini hapo.
No comments:
Post a Comment