We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, June 6, 2019

Kigogo mwingine wa CUF ajiunga na ACT Wazalendo


Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Vijana CUF Taifa (JUVICUF) Mbaraka Ismaili Chilumba ambaye uteuzi wake umefanywa hivi karibuni na Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, ametangaza kujiengua na CUF na kujiunga na chama cha ACT Wazalendo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi na Shaweji Mketo aliyewahi kuwa Kiongozi mwandamizi wa CUF ambaye naye alijiunga na ACT Wazalendo sambamba na Maalim Seif Sharif Hamad, Chilumba amesema amejiengua na CUF kwa sababu haoni mwelekeo wa chama hicho.

"Sioni mwelekeo wa CUF. Nilidhani kwamba baada ya mgogoro kwisha CUF tutajikita katika kuimarisha taswira ya chama chetu ambayo kwa kweli imeharibika sana kutokana na mgogoro na mwenendo wa viongozi wetu. Sioni jitihada yoyote ya viongozi kurejesha imani ya wananchi kwa chama chetu ambayo kwa kweli imepotea kwa kiwango kikubwa"

Alipoulizwa kwa nini amechagua kujiunga na ACT Wazalendo, Chilumba ambaye hivi karibuni alikiwakilisha chama kwenye uangalizi wa uchaguzi wa wabunge wa Jumuiya ya Ulaya katika nchi za Ubelgiji na Ujerumani alisema kuwa anavutiwa na siasa za masuala za chama hicho hasa mchango wake katika kuwatetea wakulima wa korosho.

"Kwa muda mrefu ACT Wazalendo na kiongozi wake Mh. Zitto Kabwe wameshiriki ndani na nje ya bunge kuwatetea wakulima wa korosho na makundi mbalimbali Kusini na Tanzania kwa ujumla. Ninaamini hiki ni chama sahihi kwangu"

Alipohojiwa kama ana mpango wowote wa kugombea ubunge 2020, Chilumba ambaye ni msomi anayechukua shahada ya pili yaani Masters in Entrepreneurship and Enterprise Development katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM alisema "Wakati utaamua. Kwa sasa ninataka kushiriki kikamilifu kukijenga chama changu kipya kwetu Newala na Tanzania kwa hali na mali".

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list