Licha ya kutangulia mara mbili, timu ya Taifa ya Tanzania imepoteza mchezo dhidi ya Kenya baada ya kufungwa mabao 3-2
Bao la mapema dakika ya sita lililofungwa na Saimon Msuva liliipa matumaini Stars ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo
Hata hivyo mipira ya juu iliyokuwa ikitumiwa na Kenya, ilisababisha matatizo langoni kwa Stars mara kwa mara na Kenya ilifanikiwa kusawazisha bao hilo kwenye dakika ya 38 likifungwa na Michael Olunga
Dakika moja baadae, juhudi za nahodha Mbwana Samatta ziliiwezesha Stars kupata bao la pili kwenye dakika ya 39
Hata hivyo Kenya ilikuwa imara zaidi kwenye kipindi cha pili ikifanikiwa kufunga mabao mawili yaliyoihakikishia ushindi kupitia kwa Johanna Omolo na Michael Olunga
Kenya ilitumia zaidi mipira ya juu ambayo iliwasumbua walinzi wa kati wa Stars pamoja na mlinda lango Aishi Manula
Matokeo hayo yameiondoa Stars kwenye michuano hiyo huku Kenya ikiwa na nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora ikihitaji angalau alama moja mchezo dhidi ya Senegal
Stars itakamilisha ratiba kwa kuumana na Algeria jumatatu.
No comments:
Post a Comment