Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stagomena Tax katika kikao cha awali cha mashauriano kuhusu mkutano wa SADC.
Mkutano huo wa SADC unaotarajiwa kufanyika nchini Tanzania, Agosti mwaka huu ambapo Tanzania atakabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Jumuiya hiyo baada ya miaka 16 ambapo Rais Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Akizungumza hivi karibuni na vyombo vya habari jijini Dar es salaam, Msemaji wa Serikali Dk.Abbasi amezungumzia ziara alizofanya Rais Magufuli kwa baadhi ya nchi jirani kuwa ni moja ya maandalizi ya mkutano huo.
"Ziara hii Rais ameifanya ikiwa ni maandalizi ya kuchukua Uenyekiti wa SADC Julai mwaka huu, na Agosti tutakuwa na mkutano wa Marais wa SADC na Tanzania itakuwa mwenyeji, alikwenda Namibia kukutana na Mwenyekiti anayemaliza muda wake, mara ya mwisho Tanzania kushika uenyekiti SADC ilikuwa miaka 16 iliyopita", amesema.
No comments:
Post a Comment