Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinaondoka leo kuelekea nchini Misri kuendelea na maandalizi ya michuano ya AFCON 2019 inayotarajiwa kuanza Juni 21 2019
Kocha Mkuu wa Stars Emmanuel Amunike leo atatangaza majina ya wachezaji 32 ambao wataondoka na timu hiyo
Kikosi cha wachezaji 23 ndicho kitakachoshiriki michuano hiyo, hivyo wachezaji wengine tisa watachujwa baada ya kambi hiyo kumalizika
Jana Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza alimkabidhi bendera nahodha wa Strs Mbwana Samatta kwenye hafla iliyofanyika Hotel ya Whitesands ilipo kambi ya Stars
No comments:
Post a Comment