Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba hawatashiriki michuano ya CECAFA Kagame Cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 07 mpaka Julai 21 nchini Rwanda, imefahamika
Simba na Azam ndio timu pekee zilizotarajiwa kushiriki michuano hiyo kutoka Tanzania Bara kabla ya Yanga kupewa mwaliko
Mtendaji wa Sima Crescentius Magori amesema wamelazimika kujitoa kwenye michuano hiyo kutokana na sababu za kiufundi
Amesema mabadiliko ya ratiba ya ligi ya Mabingwa msimu ujao yamewalazimu kujiondoa kwenye michuano hiyo
Hatua ya awali ya michuano hiyo inatarajia kuanza mwanzoni mwa mwezi wa nane, hivyo hakutakuwa na muda mrefu wa kufanya maandalizi
Magori amesema tayari wameitaarifu TFF juu uamuzi huo wakujitoa
No comments:
Post a Comment