Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amepinga wazo la kutafutiwa Kocha Msaidizi mzawa akisisitiza kwa sasa anaridhika kufanya kazi na Noel Mwandila
Inaelezwa uongozi wa Yanga ulikuwa mbioni kumalizana na kocha wa Kagera Sugar Meckie Mexime kuwa kocha Msaidizi huku timu hiyo ikipanga kumrejesha Mwandila kwenye majukumu yake ya kocha wa viungo
Hata hivyo Zahera ameonyesha kutokuwa tayari kufanya kazi na kocha mzawa licha ya kutambua wapo makocha wazawa wenye uwezo mkubwa na anawaheshimu
Lakini amesema kutokana na tabia za wachezaji wa Kitanzania, wakiongozwa na kocha mzawa kutakuwa na changamoto
"Mimi mwenyewe ndio napaswa kutafuta Kocha Msaidizi," amesema Zahera ambaye yuko nchini Hispania kwenye kambi ya timu ya Taifa ya DR Congo
"Nimeridhika kufanya kazi na Mwandila ni kocha mzuri na anajua mpira ndiye anafaa na ataendelea kuwa msaidizi wangu kama angekuwa hafai ningesema na kumchagua mwingine"
"Siwezi kuwa na kocha msaidizi mzawa maana tabia za wachezaji wengi wa kitanzania ni changamoto"
No comments:
Post a Comment