Klabu ya Brighton & Hove Albion imefanikiwa kumsajili winga wa KRC Genk ya Ubelgiji, Leandro Trossard kwa dau la pauni milioni 118 ikiwa ni mkataba wa miaka minne kuitumikia timu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Trossard mwenye umri wa miaka 24 amejiunga na Brighton hapo jana siku ya Jumatano akitokea ligi ya Ubelgiji maarufu kama Belgian Jupiler Pro League baada ya kudumu ndani ya klabu ya KRC Genk kwa miaka tisa huku akiipatia ubingwa akiwa pamoja na swahiba wake Mbwana Samatta.
“Nimetumia muda wangu mwingi nikiwa na timu yangu hiyo ya utotoni na kujifunza mambo mengi, ni timu yangu ya utotoni na nimezaliwa huko.“ Amesema Leandro Trossard.
“Msimu uliyopita ulikuwa mzuri ambapo nilikuwa nahodha kwa muda na kuisaidia timu yangu, nilijifunza mengi na kwasasa ninayo furaha kuja kwenye ligi kubwa kuisaidia Brighton kufikia mafanikio.”

Trossard alikuwa miongoni mwa wachezaji muhimu waliyoweza kuisaidia KRC Genk kutwaa ubingwa wa ligi, akifunga jumla ya magoli 22, akitoa pasi za mwisho 11 zilizochangia mabao ’assists’ huku akiifikisha timu hiyo kutinga hatua mtoano Europa League.
Brighton & Hove Albion ni klabu ya nchini Uingereza ambapo msimu uliyopita wa mwaka 2018/19 ilimaliza nafasi ya 17 katika timu 20 zinazoshiriki Premier League.
No comments:
Post a Comment