Beki anayetajwa kusajiliwa na Yanga Ali Mtoni 'Sonso' amesema atahakikisha anapambana ili kupata namba katika kikosi cha Mwinyi Zahera
Nahodha huyo wa Lipuli Fc anasubiri kumalizika kwa mkataba wake ili aweze kutambulishwa rasmi Yanga
"Baada ya siku mbili au tatu itafahamika kama nitacheza Yanga au la," Sonso aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya mchezo wa fainali kombe la FA uliomalizika kwa Lipuli kuchapwa bao 1-0 na Azam Fc
Aidha Sonso amesema anaamini atakuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga muhimu ni kuhakikisha anamshawishi Mwalimu kwa kujituma mazoezini
"Muhimu natakiwa nikapambane katika mazoezi kwani naamini kama nitafanya vizuri Mwalimu hataninyima nafasi"
Sonso ni miongoni mwa wachezaji walioitwa timu ya Taifa na kocha Emmanuel Amunike inayojiandaa na fainali za AFCON 2019 ikiwa imeingia kambini jana
No comments:
Post a Comment