Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Suzan Lyimo amewataka Wabunge wanawake kuandamana baada ya bajeti Kuu ya serikali kuongeza ushuru wa nywele bandia (mawigi) wa asilimia 10 kwa bidhaa za nywele bandia zinazozalishwa nchini na asilimia 25 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje nchi.
Lyimo amesema kuwa anaona bajeti hiyo haina gender balance kwanini haijatafuta bidhaa ya wanaume waiwekee kodi? wanachagua bidhaa za wanawake?
"Mawigi ni bidhaa kwaajili ya wanawake. Kuna watu "naturally" hawana nywele, wana vipilipili hivyo ni lazima wavae mawigi, nilitegemea wabunge wanawake tuandamane kupinga hii bajeti, imekuwa "gender insensitive" hasa suala la pedi kurudishiwa kodi,"alisema Lyimo.
Hata hivyo, Mbunge huyo alitoa mfano wa baadhi ya Wabunge waliovaa mawigi walivyopendeza huku akimtaka Naibu Spika kuwaangalia
We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.
Subscribe to our RSS feed to stay updated on our progress.

No comments:
Post a Comment