Club ya Liverpool ya England usiku wa June 2 2019 ilicheza mchezo wake wa fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Tottenham Hotspurs, game hiyo ilichezwa ikiwa inazikutanisha timu zote za England, Liverpool ambao wanacheza fainali ya Champions League kwa mara ya pili mfululizo walifanikiwwa kuifunga Tottenham 2-0.
Magoli ya Liverpool yakifungwa dakika ya 2 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Mohammed Salah aliyefunga baada ya kupatikana kwa penati hiyo kwa Sissoko kushika mpira katika 18, super Sub Divock Origi dakika ya 88 akafunga goli la pili lililoihakikishia Liverpool Ubingwa wa Champions League kwa mara ya sita.
Liverpool sasa inakuwa club ya tatu kwa utwaaji wa taji hilo mara nyingi (6) baada ya Real Madrid waliyopo nafasi ya kwanza kwa mataji 13 na AC Milan waliotwaa mataji 7, kwa upande wa kocha wao Jurgen Klopp anaweza historia ya kutwaa taji lake la kwanza la Champions League baada ya kuzifundisha timu za Liverpool na Dortmund na kushindwa kuchukua.
No comments:
Post a Comment