Shirikisho la soka barani Africa CAF limemuondolea adhabu ya kukosa mchezo wa kwanza wa AFCON dhidi ya Senegal mlinzi wa kulia wa Taifa Stars Hassan Kessy Ramadhan baada ya kubainika kuwa hakuwa na kadi tatu za njano kama ilivyoelezwa awali.
Akizungumza na Azam TV kocha wa Stars, Emmanuel Amunike amesema swala hilo limeshawekwa sawa baada ya TFF kuomba ufafanuzi wa adhabu hiyo na CAF wamejiridhisha kuwa Kessy yuko huru kuitumikia Stars endapo mwalimu atahitaji kumtumia kwenye mechi ya kwanza ya AFCON dhidi ya Senegal itakayochezwa Jumapili.
MICHEZO YOTE YA AFCON 2019 TUTAIRUSHA MUBASHARA KUPITIA APP HII


No comments:
Post a Comment