Muda mfupi baada ya Yanga kutangaza kutoshiriki michuano ya kombe la Kagame, Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Soka Afrika Mashariki (CECAFA), Nicholas Musonye amesema uamuzi huo wa Yanga hautaathiri chochote kwenye mashindano hayo kwa kuwa timu hiyo isingefanya maajabu
"Yanga ni timu ya ovyo. Hawakushiriki mashindano yaliyopita pia"
"Kumbuka wao sio mabingwa wa Tanzania, hatutawamiss. Acha wajitoe ndio maana wakishiriki mashindano ya CAF huwa wanafungwa mabao 5-0, 6-0, Hatujai kujiondoa kwao," Musonye amenukuliwa na mtandao wa GOAL
Kauli hiyo imewakera wadau wa soka nchini hasa Wanayanga kwani haikupaswa kutolewa na kiongozi wa ngazi ya juu kabisa kwenye soka la Afrika Mashariki
Wengi wamehoji kwa nini walitoa mwaliko kwa mabingwa hao wa Kihistoria kama walifahamu wasingeleta changamoto yoyote kwenye michuano hiyo?
Michuano ya kombe la Kagame imeendelea kupoteza umaarufu wake siku hadi siku kutokana na viongozi wa CECAFA kukosa ubunifu
Kwa miaka mingi zawadi zimeendelea kubaki hivyo hivyo huku waandaaji wake wakishindwa kuiboresha
Mfano mwaka huu ratiba ya michuano hiyo itaingiliana na michuano ya AFCON 2019 huko Misri
Ni wazi hakutakuwa na msisimko kwa kuwa mashabiki wengi watakuwa wanafuatilia michuano ya AFCON
No comments:
Post a Comment