Waziri wa wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametembelea Uwanja Mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA-TERMINAL III) kuvikagua vyombo vyake vilivyojipanga kufanya kazi katika uwanja huo unaotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.
Katika ukaguzi huo Waziri Kangi Lugola pia aliambatana na Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yake katika ziara hiyo, lengi ni kuhakikisha pindi uwanja wa ndege huo utakapokamilika kunakuwa na usalama wa kutosha.
"Moja ya miundombinu mikubwa aliyochagua kuimarisha ni ujenzi wa kiwanja cha ndege, na kama mnavyojua kiwanja hiki cha ndege tuna majeshi matatu yanayofanya kazi", - amesema Kangi
Kangi Lugola amesema ukaguzi alioufanya ameridhishwa na vyombo vyake ambavyo ni Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na uokoaji na Idara ya Uhamiaji, kuwa, wamejipanga vizuri kwa ajili ya kutoa huduma uwanjani hapo.
"Kama waziri wa Mambo ya ndani lazima eneo kama hili ili kukagua majeshi kama yako tayari 8 kutoa huduma kwenye uwanja huu kabla haujaanza kutumika" amesema Kangi Lugola.
No comments:
Post a Comment