Watu watano wamefariki na wengine watano kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na mwamba kwenye mgodi wa dhahabu wa Kilama ulioko wilayani Gairo mkoani mkoani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya hiyo Siriel Mchembe amesema tukio hilo limetokea jana tarehe 8/6/2019 baada ya wananchi wengi wao wakitokea wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, kuvamia mgodi huo hali iliyosababisha vurugu kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa “mgodi umetema”.
Amesema mnamo tarehe 2/6/2019 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ambayo yeye ni mwenyekiti wake alifika katika mgodi huo ulioko eneo la milimani takriban Kilomita 10 kutoka eneo la mji na kutoa elimu lakini bado wananchi walionekana kutofuata maelekezo waliyopewa.
“Kwa masikitiko makubwa jioni ya leo baada ya kutoka mgodini, nimepokea taarifa wananchi wanne wamefariki kwa kudondokewa na mwamba uliokuwa na dhahabu. Aidha wananchi watatu wamelazwa Hospitali ya Berega baada ya kujeruhiwa… Wananchi tutulie na tufuate maagizo ya viongozi wetu katika uchimbaji wa dhahabu KIlama,” ni sehemu ya taarifa iliyotolewa jana na mkuu huyo wa wilaya kabla ya idadi ya vifo na majeruhi kuongezeka na kufikia watano
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa wilaya waliofariki katika tukio hilo wote ni wakazi wa wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na wanne majina yao yametambuliwa kuwa ni Baraka Karoli (36), Shida Rashid (32), Samwe Paul (19) na Juma Chobala (35).
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa vifo vya watano kwenye mgodi huo na kutoa onyo kwa watu wenye nia ya kufanya uhalifu kwenye eneo hilo huku akitoa uhakika kuwa ulinzi umeimarishwa.
We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.
Subscribe to our RSS feed to stay updated on our progress.
No comments:
Post a Comment