Licha ya Simba kufanya usajili wake kwa usiri mkubwa, nyota wa Nkana Fc Walter Bwalya ni miongoni mwa wachezaji wanaowaniwa na mabingwa hao wa Tanzania Bara
Nyota huyo anayekipiga timu ya Taifa ya Zambia anawaniwa na timu kadhaa lakini Simba ina nafasi kubwa ya kumsajili
Nkana Fc haitashiriki michuano ya CAF msimu ujao hivyo ni dhahiri nyota wa timu hiyo waliofanya vizuri msimu uliopita kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho wataondoka
Mzambia huyo amebainisha kuwa yuko tayari kutua Simba kama matajiri hao wa Msimbazi watafikia nae makubaliano
Baada ya kumkosa Lazarus Kambole wa ZESCO aliyetimkia Kaizer Chiefs, Simba imedhamiria kumnasa Bwalya ili kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji
Simba ilijaribu kumsajili Bwalya wakati wa usajili wa dirisha dogo ili achukue nafasi ya Emmanuel Okwi aliyekuwa akiwaniwa na Kaizer Chiefs
No comments:
Post a Comment