We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, June 27, 2019

Hamuwezi kuendelea na maisha msiponitaja? -Nape

Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye amezungumzia kuhusiana na kutajwa katika ujumbe uliochapishwa kwenye akaunti ya kijamii ya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe.

Kupitia ukurasa wa twitter wa Zitto umechapisha ujumbe unaodai kuwa kiongozi huyo wa ACT- Wazalendo ameunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano na kuwataka viongozi wengine wa upinzani kuipongeza serikali na sio kukosoa kila kitu.
Nape ameandikwa kuwa, "Nimeona tweets zinazodaiwa kuwa za Ndugu Zitto zikinitaja, amekakanusha sio zake. Kilichonishangaza ni uwezo mdogo wa kufikiri wa wadukuaji! Mnanyimwa usingizi na nini?? Hamuwezi kuendelea na maisha msiponitaja!", amemalizia kwa kucheka.
Moja ya ujumbe uliochapishwa ambao Zitto mwenyewe pamoja na chama chake wamekanusha ujumbe huo umesema kuwa, "Wapo ambao najua wataniita majina mengi ya ajabu kwa maamuzi yangu haya kama jinsi ambavyo wamekuwa wakimshambulia ndugu yangu Nape Nnauye kwa kutokuwa na misimamo thabiti lakini nataka niwaambie huo ndio msimamo wangu na sitaki kuyumbishwa kwani hata Wanakigoma wamefaidika".
Taarifa ya chama cha ACT-Wazalendo iliyotolewa na Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi imesema kuwa taarifa zinazowekwa hivi  sasa kwenye akaunti ya Twitter ya  Kiongozi wa Chama hicho Ndugu Zitto Kabwe si zake kwani simu na laptop yake vipo mikononi mwa Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list