We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 28, 2019

'Bado tupo kwenye mashindano' - Samatta

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amesema moja ya makosa ambayo yalipelekea timu ya taifa ya Tanzania kupoteza mchezo wake wa dhidi ya Kenya, ni wachezaji wa Tanzania kushindwa kulinda ushindi ambao waliupata kwenye kipindi cha kwanza.

Nahodha Samatta amefunguka hayo nchini Misri ikiwa ni saa chache baada ya kumalizika kwa mchezo ambao Stars ilifungwa kwa taabu bao 3 -2 na kuifanya kushika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa kundi C lenye timu za Algeria, Senegal na Kenya.
"Mimi nafikiri ni timu nzima tulishindwa kulinda ushindi wetu, bado tupo kwenye mashindano naamini siku zote kuanguka ni kujifunza, sisi tupo na tunaendelea kupambana, kama Mungu yupo na sisi tunaendelea kumwamini, nadhani Watanzania tumewaangusha sana na tungeweza kuwa na matokeo chanya leo." amesema Capt. Samatta
Katika mchezo jana mabao ya Taifa Stars yalifungwa na Simon Msuva kunako dakika ya 6 huku bao la pili la Stars likifungwa na Mbwana Samatta akifunga dakika ya 40.
Mabao ya Kenya yamefungwa na Michael Olunga dakika 39,82, na Omollo.
Mechi ya mwisho wa Taifa Stars inacheza na Algeria Julai 1, 2019 ambapo nafasi pekee iliyobaki ni Taifa Stars kushinda mchezo huo, na watakuwa nafasi kubwa ya kupita kwa nafasi ya upendeleo maarufu kama Best Looser endapo atafikisha alama 3, huku akitegemea mchezo wake dhidi ya Kenya na Senegal mmoja wapo ashinde na Taifa Stars ipate ipate ushindi za zaidi ya mabao 3.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list