Gavana wa Benki Kuu (BoT), Prof. Florens Luoga amesema hakuna fedha zilizonyang’anywa kwa watu wenye maduka ya kubadili fedha wakati wa ukaguzi waliofanya.
Ameeleza hayo leo Ikulu Dar es Salaam ambapo Rais John Magufuli akizungumza na wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini.
"Hakuna fedha zilizonyang’anywa kwa watu wenye maduka ya kubadili fedha, fedha zilichukuliwa kama vielelezo kwenye uchunguzi, Wataanza kupewa majibu ya utafiti uliofanywa na watakaokutwa na shida wanatakiwa kujieleza. Aliyenyang’anywa fedha aje atuambie" amesema Prof. Florens Luoga.
Utakumbuka kuwa serikali ilifanya ukaguzi wa kushtukiza katika maduka kadhaa katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na dar es Salaam na mengi kufungwa kwa maelezo kuwa yalikuwa yakifanya kazi kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment