Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) 2018/19 kwa mwezi Mei huku Ettiene Ndayiragije ambaye ni Kocha wa KMC akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi huo.
Kagere amewashinda Bigirimana Blaise wa Alliance FC na Tariq Kiakala wa Biashara United alioingia nao fainali wakati Ndayiragije akiwashinda Patrick Aussems wa Simba na Malale Hamsini wa Alliance FC.
No comments:
Post a Comment