Mwimbaji Aika kutokea kwenye kundi la Navy Kenzo anatarajia kupata mtoto wake wa pili siku chache zijazo, Aika pamoja na Nahreelwameanika good news hizi kupitia kurasa zao za instagram huku mastaa tofautofauti wameonekana kwapongeza kwa kitu hicho.
Tayari jinsia pamoja na jina la mtoto wao wa pili limeshaachiwa hadharani, fahamu kuwa mtoto huyo wa kiume ataitwa Jamaika ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa Gold ambaye alizaliwa Jumamosi ya December 9 2017.
Nikukumbushe tu kuwa Aika na Nahreel ambao ni wasanii wanaounda Kundi la Navy Kenzowamekuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya miaka kumi hadi sasa na hatimae mwaka huu 2019 wanamkaribisha mtoto wao mwingine wa pili.
No comments:
Post a Comment