Ajibu ambaye Yanga imetangaza kuachana naye rasmi msimu ujao, atamaliza mkataba na klabu hiyo ya Jangwani Jumapili hii Juni 30 na kwenda kuanza maisha mapya ndani ya klabu ya Simba.
Habari kutoka ndani ya klabu ya Simba zimelidokeza Mwananchi kuwa tayari klabu hiyo imemalizana na mshambuliaji huyo aliyewahi kuitumikia Simba kabla ya kujiunga na Yanga na sasa anarejea tena Msimbazi.
Mmoja wa vigogo wa Simba ambaye aliomba hifadhi ya jina, alisema wanachosubiri ni mshambuliaji huyo kumaliza mkataba wake na Yanga ili wamtangaze kama mchezaji wao.
Alisema kila kitu katika usajili wa Ajibu Simba kimekamilika na amepewa Sh 80 Milioni katika usajili wake sanjari na gari la Sh 20 Milioni.
Licha ya kutotaka kuweka wazi mshahara ambao nyota huyo atalipwa, kigogo huyo amesema atalipwa mshahara mnono na klabu hiyo.
Ajibu ambaye awali alipata ofa ya kuichezea TP Mazembe lakini dili hilo likayeyuka baada ya kutoonyesha ushirikiano, alipotafutwa jana hakukanusha wala kukubali kama Simba wamempa fedha hiyo ya usajili zaidi ya kusisitiza hawezi kuzungumza usajili wake kwa sasa. “Bado mkataba wangu na Yanga haujaisha, siku mkataba wangu utakapomalizika ndipo nitaongelea maisha yangu mapya ya kisoka,” alisema Ajibu kwa kifupi.
No comments:
Post a Comment