Ahukumiwa miaka 5 jela kwa kumpiga na kumjeruhi mtoto wa miaka 2
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa mtaa wa Nyang’aka Wilayani Bariadi mkoani Simiyu, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumpiga mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka miwili na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili.
Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Pili Juma anadaiwa kumshambulia mtoto huyo kwa kipigo, kisha kumtupa kwenye matuta ya viazi yaliyojirani na nyumbani kwake mnamo tarehe 30 Mei mwaka huu majira ya saa 11 jioni.
Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya
No comments:
Post a Comment