Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa beki mkongwe Kelvin Yondani atamaliza soka lake akiwa na timu hiyo
Zahera amesema amekuwa akizungumza na Yondani mara kwa mara na hawana tofauti yoyote
"Huwa nasimulia na Yondani mara kwa mara, nawahakikishia Yondani hawezi kuondoka Yanga," Zahera akiwaambia waandishi wa habari
"Nyie waandishi mnaandika sana vitu vya uongo kuhusu usajili, mara Bangala, mara Yanga inataka kusajili mchezaji wa TP Mazembe"
"Hili la Yondani nalo ni uongo, atafia Yanga"

No comments:
Post a Comment