Mlinda lango wa Bandari Fc Farouq Shikalo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga, imefahamika
Inaelezwa Shikalo alipelekea mkataba nchini Kenya na mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya usajili ya Yanga
Moja ya sharti lililowekwa kwenye mkataba wake ni yeye kuwa mlinda lango namba moja
Shikalo alikuwa akiwindwa na Yanga tangu wakati wa usajili wa dirisha dogo ambapo mchakato wake wa usajili mwezi Disemba ulikwama dakika za majeruhi
Mlinda lango huyo yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars ambacho kinajiandaa na fainali za AFCON 2019

No comments:
Post a Comment