Yanga imejipanga kwelikweli kwa ajili ya msimu ujao.
Baada ya machungu ya takribani misimu miwili, furaha inakaribia kurejea Jangwani
Sikia hii, kocha mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amefichua kuwa wanatarajia kwenda nje ya nchi kufanya maandalizi ya msimu ujao
Maandalizi hayo yatafanyika China na yatachukua zaidi ya wiki tano
Baada ya kumalizika kwa fainali za AFCON zitakazofanyika Misri mwezi ujao, Yanga italekea China kuweka kambi

No comments:
Post a Comment