Watu 32 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametembelea kambi ya wagonjwa hao iliyopo Hospitali ya Amana na kuwataka wananchi kuzingatia usafi na kuzitaka halmashauri kuongeza faini kutoka Sh30,000 hadi Sh200,000 kwa watakao chafua mazingira.
Hadi sasa Hospitali ya Amana ina wagonjwa 13, Mwananyamala (1), Temeke (18) huku mmoja akiripotiwa kufariki dunia.

No comments:
Post a Comment