Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Romario Sports 2010 limited kwa ajili utengenezaji wa jezi za timu za Taifa.
Rais wa TFF Wallace Karia amesema kwamba kuanzia sasa wakati wowote shirikisho hilo litaanza kuwachukulia hatua watu wote ambao wanauza jezi feki.
Karia amesema mkataba huo una faida kubwa kwa TFF kwani kwa Sasa shirikisho hilo halitatumia gharama ya kununua jezi na pia watapa faida ya asilimia 15 kwa kila jezi itakayouzwa na kampuni hiyo
No comments:
Post a Comment