Tetesi za usajili Simba leo
Simba wanataka Sifa na kama dili litatiki basi Simba huenda msimu ujao ikawa na safu ya ushambuliaji ambayo itakuwa hatari Fire kama ambavyo mchekeshaji Pierre Liquid kutoka Tanzania husema.
Simba inaelezwa kuwa wapo katika mchakato wa kunasa moja ya wachezaji hatari katika klabu ya ZESCO na ligi kuu ya Zambia kiujumla kwasasa.
Simba inaelezwa kuwa katika mchakato wa kuinasa saini ya mchezaji Lazarous Kambole ambaye anashikilia rekodi ya kufunga hat trick (Magoli matatu) ndani ya dakika 5 katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika
Lazarous Kambole alifanya hivyo wakati ZESCO ikiifunga Mbabane Swallows Jumamosi 18 August 2018.
Mchezaji huyo alizaliwa mwaka 1994 na kwasasa anamiaka 25 pekee huku akiwa ni moja ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Zambia na hata dili hilo inaelezwa Simba wamesanuliwa na kupewa uhakika na Clatous Chama ambaye anajua vyema mauwezo yake.

No comments:
Post a Comment