Licha ya kuhusishwa na Simba, beki wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael ataendelea kusalia kunako klabu ya Yanga akitarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Hata hivyo Yanga huenda ikamletea Gadiel mshindani mwingine katika nafasi yake, ambapo mlinzi wa kushoto wa Rayon Sport Erick Rutanga anatajwa kuwaniwa na mabingwa hao wa kihistoria
Inaelezwa mkataba wa Rutanga na Rayon Sports umebakisha muda mfupi, utamalizika mwezi wa saba na huenda akatua Yanga baada ya mkataba huo kumalizika
Msimu huu Yanga imedhamiria kutumia vyema nafasi kumi za wachezaji wa kigeni ambapo Zahera alifichua kuwa wachezaji wote wa kigeni watakaosajiliwa ni lazima wawe wanacheza katika timu zao za Taifa
Tayari Yanga inadaiwa kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wa Kimataifa kutoka Rwanda.
Kama atasajiliwa, Rutanga atakuwa mchezaji wa tatu kutoka nchini humo

No comments:
Post a Comment